Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhubiri apokea kichapo baada ya kutabiri kwamba watu watakufa kutokana na ajali

33e2ea3ed641cb14 Mhubiri apokea kichapo baada ya kutabiri kwamba watu watakufa kutokana na ajali

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Wachuuzi katika soko ya Kaithimani kaunti ya Machako wamemshambulia mhubiri mmoja na kumpa kichapo cha mbwa baada ya kutabiri kuhusu vifo vingi kutokea eneo hilo.

Mhubiri huo anadaiwa pia kutoa utabiri wa kwanza wa aina hiyo hivi majuzi ambapo alisema kungekuwa na ajali na watu watakufa, kwa kweli utabiri huo ulitimia.

Kulingana na wachuuzi hao, ajali ilitendeka katika soko hilo na watu 2 walipoteza maisha yao na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya.

Nabii huyo ambaye huwa anahubiri katika soko hilo kila siku, alinusuriwa na maafisa wa polisi waliofika eneo la tukio.

Baadhi ya wachuuzi walimkashifu mhubiri huyo kwa kutoa utabiri wa aina hiyo badala ya kuomba na kukemea usije ukatimia.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke