Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhubiri anayedai kutatua shida za uzazi akabiliwa na kosa la ubakaji

Mhubiri Anayedai Kutatua Shida Za Uzazi Akabiliwa Na Kosa La Ubakaji Mhubiri anayedai kutatua shida za uzazi akabiliwa na kosa la ubakaji

Fri, 19 May 2023 Chanzo: Bbc

Jacob Wekesa, anayejiita nabii, amejikuta katika hali isiyofaa baada ya kukaa kwa muda wa wiki moja kwenye nyumba ya mmoja wa wafuasi wake.

Mfuasi wa shirika la Legion of Mary, anayedai kuwa na uwezo wa kutambua matatizo ya afya ya uzazi ya wanawake kwa macho yake ya kiroho, sasa anakabiliwa na mashtaka ya makosa ya kingono katika mahakama ya Nakuru, gazeti la Daily Nation limesema.

Ingawa amekanusha mashtaka ya kuwabaka mabinti wawili wa mwenyeji wake, mahakama imempata na hatia.

Mwanaume huyo anapigania kujiokoa kutokana na kifungo cha muda mrefu iwapo mahakama itashawishiwa na kesi ya upande wa mashtaka.

Masaibu yake yanasemekana kuanza siku ya mwaka mpya alipozuru nyumbani kwa mmoja wa wafuasi wake Bi Sarah Atieno katika kaunti ndogo ya Njoro kusali.

Mwanamke huyo, aliyeishi na binti zake wawili watu wazima, alimkaribisha na akakubali kumkaribisha kwa muda. Ilikuwa wakati wa kukaa kwake katika nyumba hiyo ambapo mzee huyo wa miaka 66 alidaiwa kutenda makosa ya kingono dhidi ya wanawake hao wawili mnamo Januari 5, 2023.

Daily Nationa inasema kulingana na karatasi ya mashtaka, Bw Wekesa alidaiwa kufanya mapenzi kimakusudi na wanawake hao wawili kinyume na mapenzi yao katika uwanja wa Golf Estate huko Njoro, shtaka alilokanusha.

Mmoja wa wahanga hao akitoa ushahidi wake mbele ya mahakama hiyo alisema mtu huyo aliyeletwa nyumbani na mama yake mzazi alidai kuwa ni nabii wa kanisa la Legion of Mary ambaye ni kipofu.

Chanzo: Bbc