Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhubiri aliyetaka kumpa ushuhuda Rais Ruto akamatwa

Mhubiri Aliyetaka Kumpa Ushuhuda Rais Ruto Akamatwa Mhubiri aliyetaka kumpa ushuhuda Rais Ruto akamatwa

Thu, 18 May 2023 Chanzo: Radio Jambo

Polisi katika kaunti ya Homa Bay wamemkamata kasisi mmoja ambaye alitaka kukutana na Rais William Ruto ndani ya siku 21 ili kushiriki naye unabii kuhusu mustakabali wa Kenya.

Joseph Chenge wa Kanisa la Jerusalem Mowar alikamatwa Jumatano jioni pamoja na washirika 11 katika nyumba yao ya ibada katika kijiji cha Ruri, eneo bunge la Suba Kaskazini.

Polisi waliwatia ndani wachungaji sita na watu watano waliokuwa wakikaa kanisani kwa ibada. Watuhumiwa wanazuiliwa katika Kituo cha Polisi Mbita.

Ofisa wa DCI kaika Homa Bay, Abed Kavoo alisema wanamshikilia Chenge kwa kuendeleza mafundisho ya dini kwa vitendo vinavyotia shaka.

Kavoo alisema uchunguzi wao wa awali umebaini kuwa kasisi huyo alikuwa akiwazuilia wagonjwa 'ili kuwaombea' badala ya kuwaruhusu kutafuta dawa hospitalini.

"Wagonjwa wenye magonjwa tofauti wanazuiliwa katika kanisa lake akidai kuwaombea. Wengine wamekuwa kanisani kwa zaidi ya miezi mitatu," Kavoo alisema.

Jumamosi iliyopita, klipu ya video iliyohusishwa na Chenge ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo alimwomba Rais Ruto akutane naye ndani ya siku 21 ili kutabiri.

Alidai kuwa Mungu alikuwa amemtabiria jambo kuhusu Kenya ambalo alihitaji kukutana na rais na kumwambia.

Mhubiri alionya kwamba jambo la bahati mbaya linaweza kutokea ikiwa watashindwa kukutana ndani ya muda uliowekwa.

"Pata muda tukae pamoja ili niwaelezee unabii wa Mungu. Tutaomba pamoja baadaye ili tuweze kuingilia kati," Chenge alisema.

Wengi wa wafuasi wake wanaamini kuwa Chenge ana nguvu za maombi ambazo zinaweza kuwawezesha wagonjwa kuponywa magonjwa mbalimbali.

Kavoo alisema baadhi ya wagonjwa walizuiliwa kanisani bila kuzingatia hali zao.

"Wengine walipatikana katika hali ya kusikitisha. Tunashuku walikuwa wakiombewa maombi ambayo yalibadilisha mawazo yao ya kawaida," aliongeza.

Kulingana na Kavoo, Chenge alikiuka sheria kwa kuendesha kanisa bila leseni ya usajili.

Pia alikosa leseni ya daktari ambayo inamruhusu kuponya wagonjwa.

"Kanisa halijasajiliwa. Pia anawaweka kizuizini wagonjwa kwa madhumuni ya uponyaji lakini yeye si daktari, jambo ambalo linaweka maisha yao hatarini," Kavoo alisema.

Chenge na wapambe wake watahojiwa ili kubaini ukweli wa kile kinachotokea katika kanisa lake.

"Hatukuweza kusita kumkamata kwa sababu hatujui hatua hizo zinaweza kusababisha nini. Tulichukua hatua na kuwakamata ili kuepuka majuto yoyote katika siku zijazo," Kavoo alisema.

Chanzo: Radio Jambo