Uamuzi wa kihistoria wa mahakama ya Eldoret nchini Kenya imemhukumu Humphrey Shilisia kifungo cha miaka 310 gerezani.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ,Humphrey Shilisia alipatikana na hatia kwa makosa manne ya wizi wa kutumia nguvu na moja la ubakaji.
"Mahakama ya Eldoret imemhukumu Humphrey Shilisia kifungo cha miaka 310 jela kwa makosa manne ya wizi wa kutumia nguvu na shtaka moja la ubakaji," ODPP alisema.
Uamuzi huu unakuja baada ya kesi ndefu na ya kina iliyochukua miaka kadhaa kufuatiliwa, kwa mujibu wa timu ya mashtaka, inasema mhalifu ambaye alikuwa akiingia katika nyumba za watu usiku, kuwaibia na kutumia vitisho vya vurugu na ghasia.
Katika visa fulani, alifikia hatua ya kuwabaka baadhi ya waathiriwa wake.
Mnamo 2020, Shilisia aligonga vichwa vya habari baada ya kutoroka Kituo cha Polisi cha Langas huko Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu.
Alikamatwa tena wiki mbili baadaye huko Shinyalu, kaunti ya Kakamega kufuatia taarifa kutoka kwa wananchi.