Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mhadhiri asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa kingono

Dsc Nigeria Mhadhiri asimamishwa kazi kwa unyanyasaji wa kingono

Thu, 25 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nigeria Nsukka (UNN), amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kumnyanyasa kingono mwanafunzi wa kike, taarifa ya chuo hicho imesema.

Hatua hiyo imekuja baada ya video kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikimuonesha mwanamume akiwa amevalia bukta huku akijaribu kuficha sura yake katika eneo linaloonekana kuwa ni ofisi na watu wakimzongazonga.

Katika video hiyo, mtu mmoja anasema: "Tumekuwa tukifuatilia hii kitu tangu siku ya kwanza, tuna sauti, maelezo na kila kitu."

Taarifa ya chuo imesema kwamba mhadhiri huyo amesimamishwa kazi, kusubiri matokeo ya uchunguzi wa jopo lililoundwa kuchunguza kadhia hiyo.

"Chuo Kikuu cha Nigeria hakina uvumilivu kabisa dhidi ya tabia ya unyanyasaji wa kijinsia inayohusisha wafanyikazi wetu na wanafunzi," taarifa ya chuo kikuu hicho imesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live