Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgonjwa wa pili wa Ebola DRC amefariki dunia

Ebola Kifo Kifo Mgonjwa wa pili wa Ebola DRC amefariki dunia

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mgonjwa wa pili aliyekuwa anaugua ugonjwa wa Ebola amefariki dunia huko kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa hiyo imetolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, ikiwa ni siku chache baada ya mripuko mpya wa ugonjwa huo kutokea nchini Congo.

WHO imesema uchunguzi wa vinasaba ulionyesha maambukizo mapya yalithibitishwa wiki iliyopita kutoka kwa mnyama aliyeambukizwa.

Hata hivyo, maambukizo hayo hayahusiani na mripuko wa mwisho, ambao ulitangazwa mwezi Desemba. Mgonjwa wa pili alikuwa ni mwanamke na ndugu wa mgonjwa wa kwanza.

Mgonjwa huyo alianza kuonyesha dalili za Ebola mnamo Aprili 5 lakini hakupata matibabu kwa zaidi ya wiki moja. Baadaye alilazwa katika kituo cha wagonjwa wa Ebola mjini Mbandaka na kufariki siku iliyofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live