Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgonjwa miongoni mwa raia waliouawa katika shambulio la waasi DR Congo

Mgonjwa Miongoni Mwa Raia Waliouawa Katika Shambulio La Waasi DR Congo Mgonjwa miongoni mwa raia waliouawa katika shambulio la waasi DR Congo

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Raia 10 waliuawa katika shambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na watu wanaoshukiwa kuwa waasi wa Allied Democratic Forces (ADF), ripoti zinasema.

Waasi hao walichoma moto kituo cha afya, kupora maduka na kuchoma nyumba katika kijiji jirani cha Mangodomu siku ya Jumanne, kulingana na Emmanuel Kathembo Salamu, meya wa jiji la Mangina katika jimbo la Kivu Kaskazini.

"Jeshi linawasiliana na adui. Saikolojia inatawala hapa," meya alinukuliwa akisema.

Mgonjwa katika kituo hicho cha afya aliripotiwa kuwa miongoni mwa raia waliouawa wakati wa shambulio hilo.

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado halijatoa tamko lolote kuhusu uvamizi huo.

Awali ADF ilikuwa ni kundi la kijihadi la Uganda lakini iliahidi utiifu kwa Islamic State mwaka 2019.

Miaka miwili baadaye, majeshi ya Uganda na DR Congo yalianzisha operesheni ya pamoja ya kijeshi dhidi ya ADF, lakini walishindwa kudhibiti mashambulizi yao.

Chanzo: Bbc