Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgomo wa madaktari wasitishwa nchini Kenya

Mgomo Wa Madaktari Wasitishwa Nchini Kenya Mgomo wa madaktari wasitishwa nchini Kenya

Wed, 8 May 2024 Chanzo: Bbc

Madaktari nchini Kenya wamesitisha mgomo ambao ulikuwa umelemaza mfumo wa huduma za afya nchini kwa siku 56.

Muungano wa madaktari na serikali walifikia makubaliano baada ya mazungumzo makali. Moja ya masuala yenye utata bado hayajatatuliwa.

Madaktari huo sasa wanatarajiwa kurejea kazini ndani ya saa 24 zijazo.

Hatua hiyo inawapa afuane Wakenya ambao wamekuwa wakihangaika kwa kukosa huduma za matibabu.

Serikali na chama cha madaktari wameshindwa kufikia makubaliano juu ya huduma na malipo ya madaktari tarajali, ambao ni uti wa mgongo wa mfumo wa afya ya umma.

Muungano huo unataka madaktari bingwa kulipwa dola 1,500 kwa mwezi, lakini serikali inasema inaweza kumudu kuwalipa dola 500 pekee.

Kesi hiyo sasa itaamuliwa na mahakama, kumaanisha kuwa madaktari tarajali hawakuwa kazini kwa siku 60 zijazo.

Chanzo: Bbc