Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea wa Upinzani Aongoza Kura za Urais Zambia

000 9KY2DF?fit=770%2C513&ssl=1 Mgombea wa Upinzani Aongoza Kura za Urais Zambia

Sun, 15 Aug 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

MGOMBEA  wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichelema  anaongoza wakati kura zikiendelea kuhesabiwa kufuatia uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali kati yake na rais aliyepo madarakani, Edgar Lungu, anayelalamikia uchaguzi kuharibiwa kwenye majimbo matatu muhimu kwake.

Kufuatia idadi kubwa ya watu kujitokeza kwenye upigaji kura wa siku ya Alhamisi,  Hichelema hadi jioni ya jana (Jumamosi, 14 Agosti) alikuwa anaongoza wakati asilimia 40 ya kura zikiwa zimeshahesabiwa.

Hadi hapo, Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) ilikuwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 62 kati ya 156, ambapo Hichelema alikuwa mbele kwa kura 1,024,212 dhidi ya Lungu aliyekuwa na kura 562,523.

Awali, waangalizi wa Umoja wa Ulaya walikuwa wamesema kwamba kampeni za uchaguzi huo hazikuendeshwa kwa haki na kwamba mamlaka zilitumika kumpendelea Rais Lungu.

Hii ni mara ya tatu kwa Hichelema kupambana na Rais  Lungu katika kile wachambuzi walichotabiri kwamba ungelikuwa mchuano mkali.

Chanzo: globalpublishers.co.tz