Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea mwanamke Senegal atamba na sera hizi

Mgombea Senegal Mgombea mwanamke Senegal atamba na sera hizi

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anta Babacar Ngom, mwanamke wa kwanza kugombea kiti cha urais huko Senegal amesema kuwa anataka kuiweka nchi hiyo katika njia ya viwanda na kuanzisha mfumo wa haki wa kugombea wanawake nafasi mbalimbali za uongozi wa nchi.

Wanawake 6 walikuwa miongoni mwa shakhsia 93 waliojiandikisha kugombea kiti cha urais katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika katika uchaguzi wa Machi 24.

Itambukwa kuwa, Baraza la Katiba la Senegal liliwaidhinisha wagombea 20 tu kuingia katika orodha ya mwisho na hivyo kupunguza dadi ya wagombea wanawake na kufikia wawili yaani Ngom na Rose. Hata hivyo Rose Wardini aliondolewa katika orodha ya wagombea kwa kutokuwa na ustahili wa kuwania kiti cha urais Senegal kutokana na uraia wake wa Ufaransa na hivyo kumuacha Anta Babacar Ngom kuwa mgombea pekee mwanamama katika kinyang'anyiro hicho.

Anta Ngom ambaye ni binti wa mfanyabiashara wa Kisenegali kwa jina la Babacar Ngom huku akijulikana kama" kiongozi wa viwanda" ni Mkurugenzi Mtendaji wa Sedima, Kampuni Kubwa ya Kuku katika taifa hilo la Afrika Magharibi.

Akizungumza na shirika la habari la Anadolu, mgombea huyo wa kiti cha urais Senegal ameweka wazi mipango yake ya uchaguzi, nafasi ya wanawake katika siasa za Senegal na uchaguzi wa rais ulioakhirishwa. Wakati huo huo amesisitiza kuwa kuna haja ya kushuhudiwa nyuso mpya katika siasa za Senegal hasa vijana na wanawake.

Rais Macky Sall wa Senegal ameitangaza Machi 24 kuwa tarehe mpya ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais ambao kuakhirishwa kwake kumesababisha machafuko makubwa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Rais Mack Sall wa Senegal

Baraza la Mawaziri la Serikali ya Sall lilitoa taarifa kwa vyombo vya habari tarehe 6 mwezi huu kuwa tangazo hilo lilitolewa baada ya Baraza la Katiba kuamua Jumatano iliyopita kwamba tarehe yoyote ya uchaguzi wa urais baada ya Aprili 2 ni kinyume na Katiba. Baraza la kulinda Katiba la Senegal liliweka wazi pia kuwa muda wa rais wa sasa hauwezi kuzidi tarehe pili Aprili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live