Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgombea anayesakwa kwa kumuua kwa risasi msaidizi wa mpinzani wake, ashinda Ubunge

Mbunge Wa Kenya Mgombea anayesakwa kwa mauaji ya raia ashinda Ubunge

Thu, 11 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Kimilili Didmus Wekesa Barasa ametetea kiti chake kwa tikiti ya Chama cha United Democratic Alliance katika Uchaguzi Mkuu nchini Kenya.

Bw Barasa, ambaye ametoroka kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga risasi msaidizi wa mpinzani wake Bw Brian Khaemba wa chama cha DAP-K Jumanne jioni, alipata kura 26,000 dhidi ya kura 9000 za Bw Khaemba.

Kiti cha ubunge cha Kimilili pia kilikuwa kimewavutia Bw Peter Makokha wa ODM na Bw Erastus Muchimudi wa Jubilee.

Wagombea wote wanne walioshiriki katika uchaguzi huo hawakujitokeza wakati wa zoezi la kujumlisha kura.

Mvutano ulikuwa mkubwa katika kituo cha kuhesabia kura za maeneo bunge katika Shule ya Upili ya Wavulana ya St Luke Kimilili Jumatano huku kukiwa na polisi wengi.

Polisi walikuwa macho kumkamata mbunge huyo ikiwa angefika katika kituo cha kujumlisha kura.

Baadhi ya wakazi wamemtetea mbunge huyo dhidi ya madai hayo, wakisema mbunge huyo alikuwa anajilinda.

“Bw Barasa alikuwa analinda, hii si mara ya kwanza kwa watu kujaribu kumuua,” akasema Bw Wasilwa Wafula.

Hapo awali, maafisa wa polisi walikuwa wamemkamata afisa msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Lwanda katika wadi ya Kimilili kwa madai ya kuvuruga kura za urais.

Hata hivyo, aliachiliwa baada ya maafisa wa IEBC na polisi kugundua kuwa kituo hicho kilikuwa na maeneo mawili ya kupigia kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: