Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wa Sudan wajadiliwa kwa kina UN

Mashambulizi Ya Droni Sudan Pengine Yalipangwa Na Waukraine  CNN Mgogoro wa Sudan wajadiliwa kwa kina UN

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kandoni mwa Kikao cha 78 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano maalumu wa serikali na mashirika ya kimataifa ili kujadili mgogoro unaonedelea sasa nchini Sudan.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Martin Griffiths, amehutubua kikao hicho cha Jumatano na kusema: "Mgogoro nchini Sudan unazidi kuwa hatari siku hadi siku, na mahitaji yanaongezeka. Jitihada zisizochoka zinafanywa kuhakikiisha misafara ya misaada inavuka mipaka hadi Darfur na kuvuka maeneo ya migogoro ndani ya nchi, lakini mchakato huo ni wa kuchosha, wa ukiritimba na wa hatari. Kilio chetu ni kupata fursa ya kufikisha misaada hiyo bila ya vikwazo na kkwa salama kwa watu ambao tunapaswa kuwafikia. Tunafanya kazi kwa bidii kupanua wigo wa kufikiasha misaada ya kibinadamu, lakini tunahitaji mchakato wa kisiasa kumaliza mapigano na kuanza kujenga upya Sudan.” Martin Griffiths

Naye Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi, amesema: “Mamilioni ya watu tayari wamelazimika kuhama makwao kutokana na vita nchini Sudan, na kila siku wanalazimika kukimbia kwenda kutafuta usalama. Wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu ili kubakia hai, lakini pia misaada ya dharura ya maendeleo ili kuweka mazingira na fursa za kuweza kuishi kwa heshima pale walipo hadi waweze kurejea nyumbani. Na zaidi ya yote, kuna haja ya kunyamazisha mtutu wa bunduki na vita hivi visivyo na maana kukoma.”

Pia akihutubu katika kikao hicho Waziri wa Nchi wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Qatar, Bi. Lolwah Rashid Al-Khater, amesema: “Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali mbaya inayoshuhudiwa nchini Sudan."

Mkutano wa Jumatano wa ngazi ya juu umeitishwa na Umoja wa Mataifa pamoja na Serikali za Misri, Qatar na Saudi Arabia, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika, AU.

Mapigano ya utumiaji silaha nchini Sudan yalianza Aprili 15 kati ya vikosi vya jeshi na vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwa lengo la kuwania madaraka, na usuluhishi wa kimataifa uliofanywa kwa madhumuni ya kuhitimisha mapigano hayo na kuzikutanisha pande mbili kwenye meza ya mazungumzo haujazaa matunda hadi sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live