Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wa Sudan umesababisha raia milioni 4.8 kuhama makazi yao

Sudan Wakimbizi Wakimbizi.jpeg Mgogoro wa Sudan umesababisha raia milioni 4.8 kuhama makazi yao

Sun, 3 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Mataifa umesema mapigano makali yanayoendelea kati ya Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) yamelazimisha mamilioni ya watu katika nchi hiyo kuyahama makazi yao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema katika ripoti yake mpya kuwa, kufikia Agosti 29, mapigano hayo yalikuwa yameshawafanya watu milioni 4.8 kuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi.

OCHA imesema, mgogoro huo umepelekea watu milioni 3 kuwa wakimbizi wa ndani (IIDPs), huku wengine zaidi ya milioni moja wakivuka mipaka na kukimbilia katika nchi jirani.

Mapigano nchini Sudan yaliyozuka Aprili 15 mwaka huu mbali na kuua watu zaidi ya 3,000, yamesababisha pia wimbi kubwa la watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kukimbilia nchi jirani ikiwemo Sudan Kusini.

Kwa mujibu wa Ofisi hiyo ya UN ya masuala ya kibinadamu, mapigano hayo yamelazimisha watu 169,060 kukimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini. UN inasema idadi ya wakimbizi wanaowasili Sudan Kusini kutokea Sudan inatabiriwa kuendelea kuongezeka kutokana na kuwa, mgogoro wa vita vya ndani huko Sudan bado haujapatiwa ufumbuzi.

Mapigano Khartoum Katika hatua nyingine, Mkuu Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ametangaza habari ya kufunguliwa mpaka baina ya nchi hiyo na jirani yake Eritrea.

Al-Burhan alitangaza hayo jana Jumamosi baada ya kuyatembelea majimbo ya Bahari Nyekundu na Kasala mashariki mwa nchi, ambapo amesisitiza kuwa vikosi vya serikali vitaendelea kukabiliana na RSF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live