Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro wa Haiti sio kipaumbele cha Kenya - Odinga

Mgogoro Wa Haiti Sio Kipaumbele Cha Kenya   Odinga Mgogoro wa Haiti sio kipaumbele cha Kenya - Odinga

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga ametilia shaka uamuzi wa nchi hiyo kuongoza ujumbe wa kulinda amani nchini Haiti ili kukabiliana na ghasia za magenge huko, akitaja kuwa ni "hatua mbaya".

Bw Odinga, katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini humo siku ya Alhamisi, alisema mpango wa kutumwa kwa polisi nchini Haiti haukuwa kipaumbele cha Kenya, akiongeza kuwa eneo la Afrika Mashariki tayari lina matatizo ya kutosha.

"Kabla hata hujafika Afrika, Haiti iko mlangoni mwa Marekani ambalo ni taifa lenye nguvu zaidi duniani. Je, ni jambo gani la kipekee kuhusu Kenya ambalo linachaguliwa kuongoza kikosi cha kimataifa nchini Haiti?" Bw Odinga alisema.

Bw Odinga alisema hali ya Haiti ni hatari, akio

Bw Odinga alisema hali ya Haiti ni hatari, akionya kwamba kupanga kutumwa kwa kikosi hicho kuna hatarisha maisha ya polisi wa Kenya.

"Majeneza yanapoanza kuwasili hapa, ndipo tutajuta. Haiti ni hatari na kuna uwezekano polisi wetu wakakumbana na matatizo huko," alisema.

“Tatizo la Haiti ni la kisiasa, halihitaji bunduki pekee, linahitaji mazungumzo,” Bw Odinga aliongeza.

Siku ya Jumatatu, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kutumwa kwa kikosi hicho kwa mwaka mmoja na hatua hiyo kupitiwa tena baada ya miezi tisa.

Rais wa Kenya William Ruto aliahidi "hatawaangusha watu wa Haiti".

Hata hivyo, baadhi ya wakosoaji wamepinga hatua hiyo, wakionyesha shaka juu ya uwezo wa polisi wa Kenya kukabiliana na magenge ya Haiti.

Chanzo: Bbc