Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro kati ya Rais na Waziri Mkuu wa Somalia wapamba moto

Somalia Mohamed Abdullahi, Rais wa Somalia

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi wa ngazi ya juu wa nchini Somali wameibua maswali na minongono mingi kwa watu kufuatia mgogoro ulioibuka kati yao juu ya sakata la uteuzi wa Mkuu wa Idara ya Usalama nchini humo.

Katika mjadala wa wazi, Rais wa nchini hiyo, Mohamed Abdullahi na Waziri mkuu Mohamed Hussein Roble, walibishana kuhusu uchunguzi wa mauji yanayoendelea nchini humo kwa takribani mwezi mmoja sasa, huku Waziri mkuu akiushtumu uongozi wa Usalama wa taifa kwa kushindwa kufanya majukumu yao ipasavyo.

Vuguvugu hilo lilichochewa zaidi mara baaya wa Waziri mkuu huyo kumtimua kazi Mkuu wa Usalam wa Taifa wa nchini humo kwa madai ya kuwa ameshindwa kutoa ripoti ya mmoja wa watumishi wa usalama aliyepotea tangu mwezi june mwaka huu, na kumteua Mkuu mpya wa Idara hiyo.

Kitendo ambacho Rais wa nchini humo aliikita kuwa ni kitendo cha kiuonevu na kinakiuka sheria pamoja na kuvunja katiba ya nchni humo, na kumteua Mkuu mwingine wa usalama, hali iliyoacha minongono mingi kwa watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live