Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mgogoro Sudan: Familia zinasubiri habari za wapendwa wao

Mgogoro Sudan: Familia Zinasubiri Habari Za Wapendwa Wao Mgogoro Sudan: Familia zinasubiri habari za wapendwa wao

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Mwanamke ambaye familia yake imenasa nchini Sudan eneo liliokumbwa na vita anasema "hajaacha kulia" wakati anasubiri habari juu yao.

Sherien Elsheikh kutoka Bristol alisema mumewe, wazazi na dada wamenaswa nchini na hawawezi kutoroka.

Zaidi ya watu 400 wamefariki katika mapigano kati ya makundi hasimu ya kijeshi nchini humo.

Serikali ya Uingereza ilisema inaanza kuwahamisha raia wa Uingereza, lakini kwa Bi Elsheikh anasema uchungu unabaki.

"[Mume wangu] amejifungia ndani ya nyumba, hawezi kutoka hata kidogo. Mama yangu, baba yangu na dada zangu - wote wapo, kwa hivyo ninahisi uchungu mwingi. "Mapigano ni karibu nao kiasi kwamba hawawezi kwenda kununua chakula.

Wanaogopa sana. "Sijaacha kulia tangu jana."

Pia kuna mfadhaiko mkubwa. Baada ya kuwasiliana na ubalozi wa Sudan mjini London, na kujaza fomu kwa matumaini kuwa zitasaidia mumewe, alisema hajasikia lolote kutoka kwa maafisa wa serikali. "Barua pepe ya uthibitisho kutoka kwao, ndivyo tu."

Kama Bi Elsheikh, Fadhalraman Mohamed kutoka Bristol pia ana wasiwasi na habari: "Mke wangu alienda huko takriban siku 25 zilizopita na alikuwa anarudi leo. "Lakini kwa kila kitu [kinaendelea], tunangojea na tunashangaa yuko wapi sasa. "Tuna watoto watano na wana wasiwasi sana. Hata asubuhi hii hawataki kwenda shule. "Kila wakati wanaendelea kutazama habari kuhusu yeye. "Inasikitisha sana na ngumu sana kwangu kufanya kazi, unajua?

Ili kuzisaidia familia, Mohammed Elsharif, kutoka Jumuiya ya Sudan ya Bristol, alisema atatafuta usaidizi kutoka kwa wabunge wa eneo hilo.

"Nitawasiliana nao wote. "Nadhani ni kupitia Ofisi ya Mambo ya Nje pekee ambapo mawasiliano yanaweza kutokea na watu hawapati majibu yoyote kutoka kwa ubalozi wa Sudan pia, kwa hivyo hali ngumu sana."

Chanzo: Bbc