Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga avamia Kanisa kuchukua tunguri alizompa mchungaji kufanya miujiza

Mganga Kanisani M Mganga avamia Kanisa kuchukua tunguri alizompa mchungaji kufanya miujiza

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Video ya mpiga ramli na washirika wake wakichukua hirizi waliyompa mchungaji imepepea mitandaoni na kuwashtua watu.

Kikosi hicho kilionekana kumpuuza mwanamke aliyejaribu kuwatuliza na kuwataka kuachana na shughuli hiyo. Kanda hiyo ilizua maoni mseto baadhi ya watu wakisema mganga huyo na kikosi chake walitaka kumtia aibu mchungaji huyo.

Mitandao ya kijamii imekumbwa na tafrani baada ya mganga mmoja na washirika wake kuvamia kanisa ili kuchukua hirizi waliyompa pasta atumie kwa huduma yake.

Kulingana na chapisho kwenye ukurasa wa X wa @eddie_wrt, tukio hilo lilitokea katika kanisa la Vision Power Ministry huko Amamole Accra mnamo Februari 22, 2024.

Video hiyo ya mtandaoni ilionyesha wakati washirika wa mpiga ramli huyo walipokuwa wakichimba sehemu ya mbele ya kanisa katika kujaribu kupata tunguri walizompa mchungahi huyo.

Wakati wakiendelea na kitendo hicho, mama mmoja wa umri wa makamo alikabiliana nao na kujaribu kuwakatizi shughuli zao, lakini walikataa na kuendelea hadi walipochukua kitu kilichokuwa kimefungwa kwenye mfuko wa plastiki unaosadikiwa kuwa ndio hirizi waliyokuwa wakiitaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live