Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mganga ajinyonga baada ya kuachwa na mkewe

MGANGA WA KIENYEJI Mganga ajinyonga baada ya kuachwa na mkewe

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Uganda wanachunguza kisa ambapo daktari wa kienyeji katika Wilaya ya Butaleja alijitoa uhai baada ya mke wake kuolewa na mwanamume mwingine.

Joseph Mwigo, mwenye umri wa miaka 38, anadaiwa kuwa na ugomvi wa kinyumbani na mke wake kabla ya kujizamisha kwenye bwawa la samaki la Ahmed Kambo Umoja siku ya Jumanne, Januari 24.

Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari nchini humo, mke wake Mwigo alikuwa ameolewa na mmoja wa wakazi katika kijiji jirani jambo ambalo lilimfanya marehemu kunywa sumu mara ya kwanza.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Busolwe mnamo Desemba 27, 2022, ambako alilazwa na baadaye aliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kupata nafuu.

Polisi waliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwigo ambaye pia alipata ulemavu wa macho mwaka mmoja uliopita, amekuwa akitishia kujitoa uhai.

Jirani wake alifichua kuwa mganga huyo alikuwa akikumbwa na msongo wa mawazo tangu mke wake alipopata mwanamume mwingine.

Mabaki ya marehemu yaliopolewa kwenye bwawa mnamo Jumanne, Januari 24, na kupelekwa katika Chumba cha kuhifadhi maiti cha Mbale City kwa uchunguzi wa maiti.

Katika kisa kingine kuhusiana na mapenzi, mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza alijiua kwa kujinyonga baada ya kukatazwa na wazazi wake dhidi ya kuwa na mpenzi au kujihusisha na mapenzi.

Lasmin Kondo wa shule ya upili ya Masaki katika Wilaya ya Kisaware kwenye mkoa wa Pwani nchini Tanzania alichukua hatua ya kujiondoa uhai baada ya onyo hilo kutoka kwa wazazi.

Akithibitisha kisa hicho, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Pius Lutumo, mwanafunzi huyo alifumaniwa na barua aliyokuwa amemwandikia mpenzi wake.

Kwa mujibu wa Lutumo, wazazi waligombeza mwanafunzi huyo na kumwonya dhidi ya kujihusisha mapenzi na akachukua maamuzi ya kujitoa uhai kwa kujinyonga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live