Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfungwa atoroka gerezani kwa kujifanya mgonjwa

Jela 1.jpeg Mfungwa atoroka gerezani kwa kujifanya mgonjwa

Tue, 13 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia mmoja wa China anayetumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la wizi katika Gereza la Nsawam, Kusini mwa Ghana ameripotiwa kutoroka alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Korle-Bu Teaching mjini Accra, kulingana na ripoti ya graphiconline.com.

Wang Xiao anaripotiwa kuwa, Jumatano wiki iliyopita alisema kuwa anaumwa, hivyo mamlaka ya magereza wakachukua jukumu la kumsafirisha hadi hospitali kwa ajili ya matibabu.

Hata hivyo, Xiao aliwakwepa maafisa wa gereza walioandamana naye wakati alipokuwa hospitalini na kutoroka, ripoti ya Graphic Online iliongeza. Tukio hilo lilitokea Jumatano, Februari 7, 2024.

Jeshi la Magereza la Ghana limethibitisha rasmi kutoroka, huku DSP Irene Pokuah Wiredu, Mkuu wa Mahusiano ya Vyombo vya Habari, akisema kuwa notisi ya mtu anayetafutwa imetolewa, inayoomba usaidizi wa umma katika kumtafuta na kumkamata tena Wang Xiao.

Mfungwa huyo ambaye awali alikamatwa Tema alisomewa mashitaka mahakamani kwa kosa la wizi na alikuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja katika Gereza la Nsawam. Zaidi ya hayo, ripoti zinaonyesha kwamba Wang Xiao anakabiliwa na mashtaka ya ziada katika kesi tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live