Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfungwa anaswa akitoroka gerezani mara ya 12

1a46010fb88ca86f Mfungwa anaswa akitoroka gerezani mara ya 12

Mon, 7 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 32, alisema alitoroka jela kwa sababu mfumo wa haki ulikuwa unachukua muda mrefu sana kuamua kesi yake

- Alisema amekuwa akisubiri kufunguliwa mashtaka kwa takriban miaka tisa na alitoroka kupitia ukuta wa gereza akitumia kamba

- Hii ilikuwa mara ya 12 Baye kutoroka gerezani japo mamlaka haijathibitisha madai hayo

Mfungwa mmoja kutoka nchini Senegal ambaye alitoroka gerezani Alhamisi, Juni 3, katika mji mkuu Dakar amekamatwa.

Baye Modou Fall alikamatwa katika eneo la Moussala mashariki mwa Senegal Jumamosi, Juni 5, karibu na mpaka wa taifa jirani la Mali, msemaji wa jeshi la Senegal alisema.

Mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 32, almaarufu kama ”mtoro sugu ” aliiambia televisheni ya Senegal kwamba alitoroka jela kwa sababu mfumo wa haki ulikuwa unachukua muda mrefu sana kuamua kesi yake.

Alisema amekuwa akisubiri kufunguliwa mashtaka kwa takriban miaka tisa na alitoroka kupitia ukuta wa gereza akitumia kamba.

Alielezea jinsi alivunja kifaa kinachoingiza hewa ndani ya seli ya mahabusu na kupanda juu ya ukuta akitumia kamba.

Baye ambaye anadai kuwa ni mfanyabiashara ambaye alirithi mali ya marehemu baba yake, amekuwa akiingia na kutoka jela tangu alipokuwa mtoto mdogo kutokana na tuhuma za wizi.

Lakini anashikilia kwamba hana fujo na wala hatumii silaha.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, hii ilikuwa mara ya 12 Baye kutoroka gerezani japo mamlaka haijathibitisha madai hayo.

Hata hivyo, wakili wake wa zamani, Abdoulaye Babou alisema huenda ametoroka karibu mara 10.

Japo mfungwa huyo anasisitiza kuwa hakusaidiwa na yeyote kutoroka gerezani, mamlaka ya gereza hiyo inasema alikuwa katika eneo lenye usalama mkali na ni lazima alisaidiwa kutoroka.

Maafisa wanachunguza iwapo kuna mtu aliyemsaidia kutoroka na wameanza kuwahoji walinzi waliokuwa zamu siku ya tukio hilo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke