Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyakazi wa soko la machinjo auawa kwa kukufuru dini

Mfanyakazi Wa Soko La Machinjo Auawa Kwa Kukufuru Dini Mfanyakazi wa soko la machinjo auawa kwa kukufuru dini

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: Voa

Usman Buda, mfanyakazi katika soko la machinjo aliuawa Jumapili katika wilaya ya Gwandu ya jimbo la Sokoto baada ya kumkufuru mtukufu Mtume Muhammad wakati wa ugomvi na mfanyabiashara mwingine katika soko hilo, msemaji wa polisi Ahmad Rufa'i alisema katika taarifa Jumapili usiku

Mtu mmoja alipigwa mawe hadi kufa baada ya kutuhumiwa kwa kukufuru huko kaskazini magharibi mwa Nigeria mamlaka na wanaharakati wamesema na kuzusha hasira siku ya Jumatatu kutoka kwa makundi ya haki za binadamu yanayohofia kile walichosema ni vitisho vinavyoongezeka kwa uhuru wa kidini katika eneo hilo.

Usman Buda, mfanyakazi katika soko la machinjo aliuawa Jumapili katika wilaya ya Gwandu ya jimbo la Sokoto baada ya kumkufuru mtukufu Mtume Muhammad wakati wa ugomvi na mfanyabiashara mwingine katika soko hilo, msemaji wa polisi Ahmad Rufa'i alisema katika taarifa Jumapili usiku.

Wakazi walisambaza video zilizoonekana kutoka eneo la tukio zikionyesha umati mkubwa wa watu ambao ulijumuisha watoto wakimrushia mawe Buda aliyekuwa Kalala sakafuni huku wakimlaani. Rufa'i alisema kikosi cha polisi kilipelekwa katika eneo hilo lakini walipofika, kundi hilo lilikimbia kutoka eneo la tukio na kumuacha mwathiriwa akiwa amepoteza fahamu. Baadaye alitangazwa amekufa katika hospitali ya Usmanu Danfodiyo huko Sokoto, Rufa'i alisema.

Mauaji hayo ni mashambulizi ya hivi karibuni ambayo wanaharakati wa haki za binadamu wamesema yanatishia uhuru wa kidini katika eneo la kaskazini mwa Nigeria lenye Waislamu wengi. hubeba adhabu ya kifo chini ya sheria ya Ki-islamu katika eneo hilo. Ofisi ya Amnesty International nchini Nigeria imesema kushindwa kuhakikisha haki katika kesi kama hizo kutachochea mauaji zaidi ya kiholela.

Serikali haishughulikii suala hili kwa umakini na hilo linapaswa kubadilika, Isa Sanusi, kaimu mkurugenzi wa Amnesty International nchini Nigeria alisema.

Chanzo: Voa