Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfanyabiashara na mkewe wauawa nyumbani kwao

Grace Mong'ina Morema Mfanyabiashara na mkewe wauawa nyumbani kwao

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Kenya wanafanya uchunguzi kuhusiana na vifo vya mfanyabiashara Edward Morema Nyagechi (63) na mkewe Grace Mong'ina Morema (60) ambao waliuawa juzi nyumbani kwao katika kijiji cha Nyamakoroto, Kaunti ya Nyamira.

Wawili hao walikuwa wakiishi nchini Marekani na walikuwa Kenya kwa ajili ya mapumziko.

Marehemu walikutwa mume nje na mke chumbani wakiwa wamefungwa mikono na miguu kwa waya huku wakiwa na majeraha ya kukatwa mapanga kichwani na shingoni, vilevile wote walikuwa wamejaziwa vipande vya nguo midomoni.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wawili hao waliteswa sana na walifariki baada ya kupoteza damu nyingi.

Wasaidizi wao wawili wa ndani na nje ya nyumba wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano. Matukio ya aina hii yamekuwa mengi kwenye ukanda huo katika siku za karibuni na yanahusishwa na migogoro ya ardhi ambapo majambazi hukodiwa ili kufanya mashambulio.

Mipango ya mazishi inaendelea huku ikiwangojea watoto wa marehemu wanaoishi Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live