Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme wa Zulu Afrika Kusini alishwa sumu, alazwa

Mfalme Wa Zulu Afrika Kusini Alishwa Sumu, Alazwa Mfalme wa Zulu Afrika Kusini alishwa sumu, alazwa

Sun, 2 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Mfalme wa Zulu wa Afrika Kusini Misuzulu kaZwelithini amelazwa hospitalini kwa tuhuma za kuwekewa sumu, waziri mkuu wake wa jadi amesema.

Mfalme huyo alitafuta matibabu nchini Eswatini kwa kuwa hana imani ya kutafuta matibabu nchini Afrika Kusini, Chifu Mangosuthu Buthelezi aliongeza.

Hii inafuatia kifo cha ghafla cha mmoja wa washauri wake wakuu, ambaye pia anashukiwa kuwekewa sumu, Chifu Buthelezi alisema.

Mfalme Misuzulu alitawazwa mbele ya maelfu ya raia wake Oktoba mwaka jana.

Lakini mzozo mkali wa kuwania madaraka umekuwa ukiendelea ndani ya familia ya kifalme juu ya kutawazwa kwa mzee huyo wa miaka 48.

Mfalme wa Kizulu hana mamlaka rasmi ya kisiasa na jukumu la mfalme katika jamii pana ya Afrika Kusini kwa kiasi kikubwa ni utamaduni, lakini bado ana ushawishi mkubwa na bajeti ya kila mwaka inayofadhiliwa na serikali ya dola milioni kadhaa.

Kundi fulani ndani ya familia hiyo linapinga madai yake ya kutaka kiti cha ufalme mahakamani, likisisitiza kuwa yeye si mrithi halali wa marehemu babake, Mfalme Goodwill Zwelithini.

Wanasisitiza kuwa mwana mwingine wa marehemu Mfalme, Simakade, ndiye anafaa kuwa mfalme.

Mfalme Zwelithini alikuwa na wake sita na watoto wasiopungua 26.

Wosia wa Mfalme Zwelithini pia umepingwa mahakamani na mke wake wa kwanza, Malkia Sibongile Dlamini-Zulu, na binti zake wawili.

Mahakama ilitupilia mbali kesi yao mwaka jana, lakini walisema watakata rufaa dhidi ya uamuzi huo.

Hakuna pendekezo kwamba washiriki wowote wa familia ya kifalme wanahusika na tuhuma za kutiliwa simu kwa Mfalme Misuzulu.

Polisi wa Afrika Kusini bado hawajazungumzia madai hayo.

Katika taarifa yake, Chifu Buthelezi alisema msaidizi mwandamizi wa Mfalme Misuzulu, aliyekaa naye, "alifariki ghafla na kuna tuhuma kwamba alilishwa sumu".

"Wakati Mfalme alipoanza kujisikia vibaya, alishuku kwamba yeye pia huenda alipewa sumu.

" Mara moja alitafuta matibabu huko Eswatini. Nimefahamishwa kuwa Mfalme alihisi hayuko sawa kutafuta matibabu nchini Afrika Kusini, kwani wazazi wake wote walikuwa wamepata matibabu nchini Afrika Kusini na kufariki dunia,” Chifu Buthelezi alisema.

Chifu Buthelezi aliongeza kuwa wakati mfalme alikuwa amemteua hivi majuzi mkuu wa mawasiliano katika ofisi yake, yeye, kama waziri mkuu wa jadi, alikuwa na wajibu wa kufahamisha taifa la Wazulu kuhusu "hali hii ya wasiwasi".

"Wasiwasi wetu moja kwa moja ni ustawi wa Mfalme. Sisi kama taifa la Wazulu tunamuombea Mfalme apone haraka.

"Iwapo kutakuwa na sababu za uchunguzi zaidi, hilo litashughulikiwa na mamlaka," Chifu Buthelezi alisema.

Chanzo: Bbc