Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme wa Uswatini atuhumiwa mauaji ya kiongozi wa upinzani

Uswatini Mfalme Mfalme wa Uswatini atuhumiwa mauaji ya kiongozi wa upinzani

Wed, 25 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mauaji yaliyofanywa dhidi ya wakili wa haki za binadamu Thulani Rudolf Maseko aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake tena mbele ya familia yake tarehe 21 mwezi huu wa Januari 21, yamezua malalaiko makubwa dhidi ya mfalme wa Eswatini, Mswati III

Vyombo vya habari viliripoti Jumamosi wiki hii tarehe 21 Januaari kwamba Maseko ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa manane wa kukamkia siku hiyo ya Jumamosi na watu wasiojulikana wakiwa na silaha.

Aliuawa akiwa nyumbani kwake huko Luhleko, katika umbali wa takriban kilomita 50 kutoka makao makuu Mbabane.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uswatini, wakili huyo, mlinzi huyo alipigwa risasi dirishani akiwa ameketi na familia yake; risasi tatu zilimpiga kifuani na moja kichwani.

Maseko alikuwa mwanasheria kiongozi wa haki za binadamu na mwandishi wa maoni nchini Eswatini, ambaye alikuwa na kesi inayoendelea mahakamani dhidi ya uamuzi wa Mfalme Mswati wa tatu kubadili jina la nchi na kuipa jina la Eswatini kwa amri. Jina la nchi lilibadilishwa kutoka Swaziland na kuitwa Eswatini kwa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa 2018. Msimamo wa mwanasiasa huyo wa upinzani ulikuwa ni kwamba Mfalme hakufuata utaratibu wa katiba katika kubadilisha jina la nchi hiyo.

Kuuawa masaa machache mpinzani huyo baada ya mfalme wa nchi hiyo kuwashutumu wanaharakati wanaopinga utawala wake, kulizua maswali mengi yasiyo na majibu tangu hiyo siku ya Jumamosi.

Mashirika mengi ya kutetea haki za binadamu nchini Eswatini yanaendelea kulaani mauaji ya wakili huyo na yanasema, yamefanywa kwa amri ya Mfalme Mswati III.

Mtandao wa Mshikamano wa Swaziland (SSN) na Shirika la Kanda ya Afrika la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi wa Kimataifa (ITUC-Afrika) nayoi yametowa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka dhidi ya Mfalme Mswati, wakimtuhumu kuwa ndiye aliyeamuru mauaji ya Maseko na wanaharakati wengine wa haki za binadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live