Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Mfalme wa Shetani' mwenye wake 57 azikwa ndani ya gari Nigeria

Mfuasi Wa Shetani Simon Odo

Thu, 16 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja nchini Nigeria Simon Odo (74) maarufu kama 'mfalme wa Shetani' amezikwa ndani ya gari katika Kijiji chake kusini mashariki mwa jimbo la Enugu baada ya kifo chake.

Mashine ya gari lake ilikuwa imewashwa na wimbo wake alioupenda ulisikika katika gari hilo, ambalo lilihudumu kama jeneza lake , kulingana na wale waliokuwepo.

'Yalikuwa mazishi ya kwanza ya aina hiyo kufanyika katika Kijiji cha Aji, walisema wakazi. Bwana Odo aliomba kuzikwa hivyo' , alisema mwanawe Uchema Odo.

Mazishi hayo ya gari lililokuwa likinguruma yaliashiria kusafiri kwake hadi ulimwengu mwengine , baadhi ya wanawe walisema.

Baadhi ya watu wa familia yake waliohojiwa walisema kwamba bwana Odo alikuwa mtu mzuri ambaye alipinga maovu wakati alipokuwa akishirikiana na watu.

Mtoto wake wa kiume Uchenna Odo alisema baba yake alifariki mwendo wa saa tisa asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Taarifa ya kifo cha "Mfalme wa Shetani" ilitolewa na mwanae Uchenna Odo kwa njia ya simu katika shirika la habari la BBC.

Wakati wa mahojiano na BBC Igbo mwaka 2020, alisema alikuwa na wake 57 na hakufahamu idadi kamili ya watoto wake zake walimzalia na hata wajukuu.

Alisema alirithi ushetani kutoka kwa wazazi wake na mababu amboa pia walikuwa ni waabudu shetani.

Anasema watu kutoka sehemu tofauti huzuru madhabahu yake kila wakati kupata ushauri ya kiroho ambao anasema hutenda vitendo vinavyowadhuru binadamu wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live