Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme wa Morocco aamuru kuachiliwa kwa Mwandishi wa Habari

Mfalme V1 Mfalme Mohammed VI wa Morocco

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme Mohammed VI wa Morocco jana aliamuru kuachiliwa kwa Waandishi wa habari waliofungwa Taoufik Bouachrine, Omar Radi na Soulaimane Raisouni kama sehemu ya msamaha uliowanufaisha wafungwa 2,476.

Katiba ya Morocco inatoa haki kwa Mfalme kusamehe au kubadilisha hukumu, uamuzi ambao kawaida huchukuliwa siku za kitaifa.

Wanahabari hao watatu walikuwa wakosoaji wakubwa wa sera za umma na wote walikuwa wamehukumiwa kwa makosa yakiwemo ya unyanyasaji wa kijinsia, ambayo walikanusha.

Watetezi wa haki za binadamu walikuwa wameshutumu kesi zao kama zilichochewa kisiasa.

Mhariri Mkuu Taoufiq Boachrine alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela mwaka wa 2018, Omar Radi na Soulaimane Raisouni wote walihukumiwa mwaka 2021 hadi miaka 6 na miaka 5.

Mfalme pia aliwasamehe wafungwa 16 waliopatikana na hatia kwa tuhuma za itikadi kali na ugaidi baada ya kuchunguza mienendo yao, Wizara ya Sheria ya Morocco imesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live