Mfalme wa Wazulu, mkuu wa ufalme wa kitamaduni wenye ushawishi mkubwa zaidi wa Afrika Kusini, alisema siku ya Jumatatu “alikuwa sawa,” na akakanusha uvumi kwamba alilishwa sumu.
“Niko vizuri sana, niko fiti sana na nina sauti nzuri,” alisema
Misuzulu Kazwelithini aliambia shirika la habari la AFP katika mahojiano ya simu kutoka nchi jirani ya Eswatini, ambako anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, kwamba hali yake ya afya ni shwari.
Kazwelithini, maarufu kama Zulu, mwenye umri wa miaka 48, alichukua usukani mwaka jana, kufuatia mzozoz mkali kuhusu urithi wa kifalme, baada ya kifo cha babake, Goodwill Zweli-thini.
Mwishoni mwa wiki, waziri mkuu wa Zulu mwenye ushawishi mkubwa, Mwanamfalme Mangosuthu Buthelezi, alisema kuwa mfalme huyo amelazwa hospitalini nchini Eswatini baada ya kuugua.
Buthelezi alisema kulikuwa na “tuhuma kwamba alipewa sumu,” baada ya kifo kisichotarajiwa cha mmoja wa washauri wake wa karibu. Mfalme Kazwelithini alikanusha ripoti za kulazwa hospitalini, alipozungumza na AFP.