Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme Mswati III aingia mafichoni huku raia wakiendelea kugoma

8382b7e56b6eaed0 Mfalme Mswati III aingia mafichoni huku raia wakiendelea kugoma

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mfalme Mswati III ameingia mafichoni huku maandamano yakiendelea kupamba moto dhidi ya utawala wake Mswati amekuwa mamlakani tangu kutawazwa Mfalme mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 18

Mfalme Mswati III wa Eswatini anaripotiwa kukimbia taifa lake kufuatia maandamano yanayoendelea.

Maandamano hayo yanadaiwa kuchochewa na kile waandamanaji walitaja kama 'ufalme wa kale' lakini bado taarifa zaidi hazijatolewa.

Ripoti ambazo hazijathibitishwa zinadai kuwa waandamanaji waliteketeza majengo kadhaa na biashara mjini Matsapha huku hali ya wasiwasi ikitanda.

Shirika la SABC linaripoti kuwa watu kadhaa pia wamejeruhiwa katika maandamano hayo ambayo yanalenga kumng'oa Mswati, ambaye alitawazwa mwanamfalme mwaka 1983 na kisha kuwa mfalme rasmi miaka mitatu baadaye akiwa na umri wa miaka 18.

Swaziland yabadilisha jina kuwa EswatiniKando na kuwa mfalme wa Swazi, Mswati anafahamika kuwa mtu wa wake wengi ambapo alimuoa mke wake wa 14 ambaye ni bikira mwenye umri wa miaka 19, miaka mitatu iliyopita.

Hii ni kulingana na tamaduni na desturi ya Swazi ambapo Mfalme anaruhuswa kuoa wasichana bikira kila mwaka akiwa mamlakani.

Kufikia sasa Mflame Mswati III ametengana na wake zake watau na kuzaa watoto 30.

Habari kuhusu wakeza hajuliakni kufuata kutoweka kwa mfalme huyo.

mengi kufuata.....

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke