Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme Charles wa tatu alivyokutana na rais Ruto

Ruto Charles.png Mfalme Charles wa tatu alivyokutana na rais Ruto

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme wa Uingereza Charles wa tatu ameanza ziara ya siku nne nchini Kenya, ziara yake ya kwanza katika koloni ya zamani ya Uingereza.

Akiwa ameandamana na Malkia Camilla, Charles aliwasili katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki usiku wa kuamkia leo ambapo amepokelewa na rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Kasri la Buckingham imesema ziara hiyo ni ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili katika maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya usalama.

Charles anatarajiwa pia kukutana na wajasiriamali kutoka eneo lenye shughuli nyingi za kiteknolojia nchini Kenya na kutembelea vituo vya wanyamapori.

Yeye na Camilla pia watasafiri hadi kusini mashariki mwa mji wa bandari wa Mombasa.

Wakenya wengi, hata hivyo, wanaangazia zaidi kile Charles atakachosema kuhusu dhuluma za wakati wa ukoloni, ikiwa ni pamoja na mateso, mauaji na kuenea kwa unyakuzi wa ardhi, ambayo sehemu kubwa bado inamilikiwa na raia na makampuni ya Uingereza.

Tume ya haki za kibinadamu nchini Kenya (KHRC) imekadiria kuwa raia 90,000 wa Kenya waliuawa au kujeruhiwa vibaya na 160,000 kuzuiliwa wakati wa mapambano ya uhuru kati ya wapiganaji wa Mau Mau na serikali ya Uingereza wakati huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live