Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfalme Charles: Hakuna kisingizio madhara ya ukoloni Kenya

Ruto Charles.png Mfalme Charles: Hakuna kisingizio madhara ya ukoloni Kenya

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfalme wa Uingereza Charles wa tatu anaeendelea na ziara yake nchini Kenya, amesema hakuna sababu inayoweza kuunga mkono mateso waliyoyapitia Wakenya wakati wa kipindi cha ukoloni, kabla ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1963.

Mfalme Charles wa tatu, ametoa kauli hiyo jana jioni wakati wa dhifa ya taufa iliyoandaliwa kwa heshima yake na rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Licha ya kuelezea masikitiko yake, kuhusu madhila waliyopata wakenya ikiwa ni pamoja na mauaji, mateso, kuzuiwa bila kushtakiwa, kupokonywa mashamba yao miongoni mwa mengine, hakuomba radhi kwa yaliyotokea kipindi chote cha ukoloni licha ya shinikizo kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu.

Naye William Ruto, amesema hatua ya Uingereza kutambua madhila hiyo inatia moyo na kutaka uimarishwaji wa uhusiano kati ya nchi hizo mbili, licha ya historia ngumu wakati wa ukoloni.

Mwaka 2013 baada ya wapigania uhuru wa Kenya Mau Mau kuishtaki Uingereza Mahakamani jijini London, serikali nchini humo ilikubali kuwalipa fidia Pauni Milioni 20. Wakenya zaidi ya 5,000 walioteswa wakati wa ukoloni.

Mfalme Charles wa tatu anatamatisha ziara yake jijini Nairobi leo kabla ya kuelekea katika jiji la Mombasa, Pwani ya nchi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live