Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu mwanamke anayegombea Urais Senegal

Mgombea Senegal Mfahamu mwanamke anayegombea Urais Senegal

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke pekee anayewania kiti cha urais nchini Senegal, Anta Babacar Ngom, anaweza asipewe nafasi kubwa sana ya kuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwishoni mwa juma hili, lakini harakati zake zimesaidia kuongeza matumaini kwa wanawake walio wengi nchini humo.

Anta mwenye umri wa miaka 40, amekuwa sauti ya wanawake na vijana wanaokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi, ukosefu wa ajira na kupanda kwa gharama ya maisha, akiahidi kutengeneza mamilioni ya ajira ikiwa atachaguliwa.

Ni watu wachache wanampa nafasi mgombea huyu kuchaguliwa miongoni mwa vinara wanaopewa nafasi, lakini wanaharakati wanasema, ukweli kwamba amekuwa mwanamke wa Kwanza kuwania nafasi hiyo baada ya mwongo mmoja, inaoneshawanawake wanapiga hatua.

Licha ya vikwazo anavyopitia kama mwanamke kutokana na tamaduni za nchi za Afrika Magharibi, Anta, amekuwa mfano wa wanasiasa wanawake ambao wamejipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii, kutokana na kuzungumzia masuala ambayo aghalabu hayajadiliwi na jamii ya Wasenegali.

Ni mwaka 2001 na 2012 Senegal ilipata mwanamke wa kwanza kuhudumu katika nafasi ya waziri mkuu, sheria ikitaka vyama kuzingatia usawa wa kijinsia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live