Mkuu mpya wa jeshi la Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore, ndiye kiongozi mdogo zaidi wa eneo hilo na mwanajeshi mwenye mkakamavu ambaye amekuwa akikosoa zaidi "mikakati isiyofanikiwa" ya mtangulizi wake dhidi ya Islamic State na wanamgambo wa al-Qaeda.
Kapteni Traore alimpindua Luteni Kanali Paul-Henri Damiba tarehe 30 Septemba, ikiwa ni mapinduzi ya pili ya kijeshi mwaka huu ambayo yanaweza kupunguza kasi ya mpito kuelekea utawala wa kiraia.
Traore, mwenye umri wa miaka 34, alianza kazi yake ya kijeshi mwaka wa 2009 na amehudumu katika vikosi mbalimbali mashariki na kaskazini mwa Burkina Faso.
Alikuwa miongoni mwa kundi la wanajeshi waliounga mkono mapinduzi ya Damiba ya Januari 24 dhidi ya Rais aliyechaguliwa kidemokrasia Roch Marc Kabore.
Hata hivyo, miezi minane baadaye, migawanyiko iliibuka katika serikali kuu inayojulikana kama Vuguvugu la Patriotic for Preservation and Restoration (MPSR).
Mbinu mbalimbali zilizotumiwa na utawala wa muda wa kijeshi wa Kanali Damiba - ikiwa ni pamoja na mageuzi kwa jeshi linalounga mkono jeshi la kujilinda, uteuzi wa magavana wa kijeshi katika maeneo yenye ghasia na kuongezeka kwa operesheni kaskazini na mashariki - zimeshindwa kuzuia mashambulizi mabaya ya wanamgambo dhidi ya raia na usalama.
Kulingana na wachambuzi wa data za migogoro ACLED Info, Burkina Faso ilichukua nafasi ya nchi jirani ya Mali kama kitovu cha ghasia za wanamgambo mwaka huu, na kusababisha maandamano ya kumtaka Damiba ajiuzulu.
Wakati mapinduzi ya kijeshi yalikuwa ya kushangaza, jeshi la Burkina Faso kwa muda mrefu limekuwa na hali ya kutoaminiana na kutoridhika tangu mapinduzi yaliyoshindwa ya 2015 ambayo yalisababisha kusambaratishwa kwa jeshi la wasomi.
Maadili ya vikosi vya usalama yameathiriwa zaidi na mashambulizi ya mara kwa mara ya waasi na mazingira duni ya kazi, hasa katika maeneo ya mipakani yenye hali tete.
Mara tu baada ya kunyakua madaraka kwa Capt Traore, vita vya maneno vilianza kati ya kikundi chake na kile cha Damiba, na kuzua hofu ya mzozo mkali wa madaraka.
Kujiuzulu kwa Damiba tarehe 2 Oktoba kulimweka Traore kuwa msimamizi wa jeshi lililogawanyika linalojitahidi kukabiliana na uasi wa kikatili ambao unaendelea kuyumbisha sehemu kubwa za Burkina Faso na Sahel pana
Mambo Muhimu
Kapteni Traore anahitaji kuliunganisha jeshi ambalo liligawanyika pakubwa na mapinduzi ya 2015 yaliyofeli
Kapteni Traore alizaliwa mwaka wa 1988 na alianza elimu yake huko Bondokuy, mji wa jimbo la magharibi la Mouhoun.
Kisha akahamia jiji la pili la nchi hiyo, Bobo-Dioulasso, kwa ajili ya elimu yake ya shule ya upili.
Akiwa katika shule ya upili, Traore alielezewa kuwa "mwenye haya na siri " lakini "mwenye akili nyingi sana".
Chama cha Muslim Pupils and Students of Burkina (AEEMB) kilisema pia alikuwa "kijana mtulivu sana".
Mnamo 2006, alijiunga na Chuo Kikuu cha Joseph Ki-Zerbo katika mji mkuu, Ouagadougou ambapo alihitimu kwa heshima ya juu, kisha akafunzwa katika Chuo cha Georges Namoano katika mji wa kusini-kati wa Po.
Traore alijiunga na jeshi mwaka wa 2009 na kupata cheo chake cha kwanza miaka miwili baadaye. Pia alichukua mafunzo ya upigaji risasi nchini Morocco.
Kisha alihamishiwa katika kikosi cha silaha huko Kaya katika Mkoa wa Kati-Kaskazini.
Alipandishwa cheo hadi kuwa luteni mwaka wa 2014.
Traore baadaye alihudumu katika ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Mali - unaojulikana kwa ufupi kwa lugha ya Kifaransa kuwa Minusma - na inasemekana alikuwa miongoni mwa walinda amani ambao "walionyesha ushujaa" kukabiliana na "shambulio tata" la wanamgambo katika Mkoa wa Timbuktu kaskazini mwa Aprili 2018. .
Mnamo 2019, Traore alishiriki katika operesheni ya kijeshi iliyopewa jina la "Otapuanu" mashariki mwa Burkina Faso iliosabbaisha utulivu kwa miezi saba. Pia alihudumu katika kikosi cha Markoye kaskazini mwa Mkoa wa Sahel na kushiriki katika operesheni kadhaa kaskazini.
Mnamo 2020, alipandishwa cheo na kuwa kapteni.
Tangu Machi, Traore amekuwa mkuu wa kikosi cha silaha kilichoko Kaya.
Kwa maneno yake mwenyewe
‘’Makubaliano yetu kwa Pamoja yamesalitiwa na kiongozi wetu kwa jina luteni kanalii paul henri Damiba. Kuzorota kwa hali ya usalama , hali iliotufanya kuchukua hatua , imetupiliwa mbali kutokana nah atua za kisiasa’’.- Septemba 30 2022 na kituo cha Habari cha serikali RTB TV.
‘’Sikuamua kuchuku madaraka, nilichaguliwa. Ni hali ambayo imekuwa ikitokota kwa wiki tatu sasa. Nilikaa kwa takriban wiki moja mjini Ouagadougou nikijadiliana naye. Lakini hakuna lililojiri. Na raia wanaona mkono anaochukua kisiasa…tulipendekeza suluhu chungu nzima na nikaelewa mwishoni , tunacheza siasa badala ya kile kilichotuleta.’’.- Oktoba 2 2022 katika idhaa ya VOA ya Ufaransa.
‘’Najua kwamba Ufaransa haiwezi kuingilia moja kwa moja masuala yetu ya ndani. Iwapo tuna washirika wengine wanaowea kutuunga mkono , sio Urusi. Wamarekani ni washirika wetu lakini pia tunaweza kushirikiana na Urusi, hivyobasi sio kuhusu Ufaransa au tatizo la Urusi na Wagner,’’ Oktoba 2 2022 katika chombo cha Habari cha France 24.
‘’Najua mimi nina umri mdogo sana zaidi ya wengi wenu hapa. Hatukutaka kilichotokea lakini hatukuwa na chaguo… kwa siku chache zilizopita , tumeusumbua usingizi wenu, tumesumbua usingizi wa wakaazi wa Ouaga kwa milio ya risasi.
"Hatukutaka hilo kiufanyika, lakini haya ndio Maisha…katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, lazima tufanye kile ambacho kilipaswa kufanywa 4katika kipindi cha miezi minane iliopita…kila kitu ni dharura," Oktoba 2 2022 akizungumza na maafisa wa wizara mbalimbali.
Kile ambacho wengine wanasema
‘’Ni miongoni mwa maafisa wenye umri wa mdogo wa jeshi ambao walihusika katika mapinduzi war ais Roch Marc Christian Kabore na kumuweka uongozini Damiba, lakini hivi sasa amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya mpito’’, gazeti la Ufaransa la Jeune Afrique lilisema Septemba 30 2022.
"Ibrahim Traore amechukua uogozi wa nchi, kama Thomas Sankar fulania, [na] mwenye umri wa miaka 34 kama yeye baada ya mapinduzi ya kijeshi. Je ipi hatma ya Burkina Faso’’..tovuti ya kibinafsi inayomilikiwa na serikali Wakat Sera ilisema Septemba 30 2022.
‘’Traore yuko karibu na wanajeshi wenzake na ni jasiri . hangeweza kuendelea bila kujiondoa’’ , chanzo kimoja ambacho hakijatajwa katika Redio ya Burkina Faso ya Omega kilisema Oktoba 1 2022.