Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mfahamu Diomaye Faye rais mteule wa Senegal

Diomaye Faye Mfahamu Diomaye Faye rais mteule wa Senegal

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bassirou Diomaye Faye rais mtarajiwa wa Senegal, ambaye amedimisha miaka 44 hapo jana, ni kiongozi ambaye mwaka mmoja uliopita raia wengi wa Senegal hawakuwa wanamtambua.

Faye amefanikiwa kuingia madarakani kutokana na ungaji mkono wa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, ambaye mamlaka ilimzuia kuwania urais licha ya kwamba aliwavutia sana vijana.

Faye alikuwa naibu wa Sonko katika chama cha Pastef, kabla ya mamlaka kukifuta chama hicho.

Kitaluma Faye amesomea maswala ya ukaguzi wa kodi na alisomea masomo hayo kwenye shule moja na Sonko na pia ametokea katika familia ambao wazazi wake walikuwa wakulima.

Aidha wawili hao walikutana katika mamlaka ya kukagua kodi nchini Senegal na ndipo wakaanzisha chama cha Pastef mwaka 2014.

Marafiki wa karibu wa Faye, wanamsimulia kama tu mwenye msimamo na asiyeshawishika kwa upesi, hilo lilimfanya kuwa ngome katika chama cha Ousmane Sonko.

Faye hata hivyo hajawahi chaguliwa katika wadhifa wowote wa kisiasa na hii ni mara yake ya kwanza kuchaguliwa, na ameahidi kuongoza Senegal kwa kuzingatia sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live