Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli yazama na kuua watu 78 Congo DR

MELI GOMA (4) Meli yazama na kuua watu 78 Congo DR

Fri, 4 Oct 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 78 wameripotiwa kufariki na wengine hawajulikani waliko baada ya meli iliyokuwa imewabeba kupinduka katika Ziwa Kivu, mashariki mwa nchi ya Congo jana Oktoba 03,2024 ambapo hadi leo jioni maiti zaidi ya 20 zilikuwa zimeopolewa.

DW Kiswahili imeripoti kuwa meli hiyo iliyokuwa imewabeba Abiria zaidi ya 250 pamoja na mizigo yao, ilizama muda mfupi kabla ya kuwasili katika Bandari Goma ikitokea kwenye Mji wa Minova katika Jimbo jirani la Kivu Kusini.

Kwa mujibu wa vyanzo vya ndani, meli hiyo iitwayo Merdy, ilipinduka kabla ya saa nne asubuhi leo kwenye Ziwa Kivu katika eneo la umbali wa karibu mita 200 kutoka kwenye soko kuu la kituku ambapo Watu wachache walionusurika walifikishwa Goma Mjini wakiwa katika hali ya mahututi na wengine walifariki muda mfupi baada ya kufikishwa Nchi kavu.

Mbali na abiria waliokuwemo, meli hiyo pia ilikuwa imebeba shehena ya chakula na vifaa vingine muhimu kutoka katika mji mdogo wa Minova na inaripotiwa kuwa Ziwa Kivu ndilo limesalia kuwa njia pekee inayotumiwa kusafirisha bidhaa kwenda katika Mji wa Goma, tangu Wapiganaji wa Kundi la M23 kufunga barabara miezi michache iliyopita.

Gavana wa Jimbo la Kivu Kusini Jean Jacques Purisi, amethibitisha taarifa hizo, na kuongeza kuwa watu 278 walikuwa wamepanda boti hiyo, kabla ya kupinduka.

"Itachukua angalau siku tatu kupata namba kamili, kwa sababu sio miili yote imepatikana," Purisi aliiambia Reuters.

Hata hivyo Gavana wa jimbo jirani la Kivu Kaskazini alisema takriban watu 58 wameokolewa.

Video fupi iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii Nchini Congo iliyorekodiwa na Mtu aliyekuwa kwenye chombo kingine cha usafiri ndani ya Ziwa Kivu, imeionesha Meli hiyo ikiwa inayumba na kulemea upande mmoja sekunde kadhaa kabla ya kupinduka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live