Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Meli ya kijeshi ya China yatua nanga Nigeria

MELI YA KIJESHI NIGERIA Meli ya kijeshi ya China yatua nanga Nigeria

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Habari Leo

Kundi la Wanamaji la Escort Task Group (ETG) 162 la China limetia nanga katika bandari ya Lagos kwa ziara rasmi nchini Nigeria.

Vyombo vya habari nchini Nigeria vimeripoti kuwa kuwasili kwa meli hiyo ya Uchina kulipokelewa kwa shangwe na maofisa kutoka Kamandi ya Jeshi la Wanamaji Magharibi, huku Afisa Mkuu wa Jeshi la Wanamaji (FOC) Rear Admiral Joseph Akpan akiongoza ujumbe huo.

Kikundi hicho kimetia nanga kikiwa na MSL Destroyer NANNING, MSL Frigate SANYA, na Supply Ship WEISHANHU, kimeingia Nigeria kwa ajili ya kusaidia kuimarisha usalama wa baharini katika eneo hilo.

Balozi wa China nchini Nigeria Bw. Chi Jian Chun ameeleza matumaini yake kuhusu ziara hiyo ambayo imepangwa kudumu kuanzia Julai 2 hadi 6 kuwa itaongeza uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Chanzo: Habari Leo