Kamanda wa polisi wa jimbo la Ogun nchini Nigeria ametangaza kuwa mchungaji wa kanisa kwa jina Peter Taiwo na mke wake, Elizabeth, watafikishwa mahakamani hivi karibuni kujibu mashitaka ya kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16 na muimbaji wa kwaya.
Msemaji wa jeshi la polisi Abimbola Oyeyemi, amesema kwamba wawili hao walihusika katika tukio la ubakaji dhidi ya msichana huyo.
Oyeyemi amesema mchungaji huyo na mke wake tayari wameomba msamaha kwa kile walichomfanyia msichana huyo mwenye umri wa miaka 16.
Msemaji wa polisi alisema kuwa mke wa mchungaji alimwambia msichana kwamba Mchungaji alimtaka usaidizi. Mara baada ya msichana kuingia ndani ya nyumba yao, mke wake alifunga mlango na ghafla mchungaji alianza mazungumzo na msichana huyo kabla ya kumbaka.
Bw Oyeyemi alisema kuwa baada ya mchungaji kumbaka msichana, mkewe alipatikana akiwa analia. Lakini mchungaji alimwambia msichana asimwambie yeyote kuhusu yaliyomtokea, kwasababu anaweza kufa. Mke wa mchungaji pia alimwambia msichana kuwa amekuwa mwanamke baada ya kushiriki ngono na mchungaji .”
Msemaji wa polisi amesema msichana huyo binafsi alipeleka malalamiko kwa polisi akidai alibakwa na mchungani alimbaka. Mahakama inatarajia kusikiliza kesi hiyo hivi karibuni, na kutoa uamuzi.