Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji maarufu Uganda anusurika jaribio la mauaji

Mchungaji Maarufu Uganda Anusurika Jaribio La Mauaji Mchungaji maarufu Uganda anusurika jaribio la mauaji

Wed, 3 Jan 2024 Chanzo: Bbc

Kiongozi mashuhuri wa kidini nchini Uganda na mfanyabiashara Aloysius Bugingo amenusurika kifo wakati wa shambulio la watu wasiojulikana na kupelekea kuuwawa kwa mlinzi wake katika mji mkuu wa Kampala.

Watu hao wenye silaha walilifyatulia risasi gari la Mchungaji Bugingo alipokuwa akienda nyumbani kwake Jumanne usiku katika eneo la Namungoona.

Washambuliaji hao baadaye walitoroka eneo la tukio kwa pikipiki.

Licha ya kupata majeraha wakati wa shambulio, Bugingo alifanikiwa kuliendesha gari hilo hadi hospitali iliyo karibu, polisi walisema.

Mlinzi wa mchungaji huyo, Richard Muhumuza, alifariki dunia kutokana na majeraha ya risasi.

"Tunapitia kwa kina picha za CCTV ili kubaini washambuliaji," polisi wameeleza.

Polisi wamesema tukio hilo ni jaribio la kuua.

Mchungaji Bugingo, mwanzilishi wa House of Prayer Ministries International, ni mfuasi mkubwa wa chama tawala nchini Uganda.

Chanzo cha shambulio hilo bado hakijajulikana.

Chanzo: Bbc