Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji auawa na majambazi Kanisani

Mchungaji Majambaziii Mchungaji auawa na majambazi Kanisani

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Wakristu waliokuwa wamekusanyika kusali katika eneo la Diepsloot, Afrika Kusini waligeuka kuwa waathiriwa wa wizi wa kimabavu baada ya majambazi kuwavamia na kumuua pasta wao.

Kulingana na ripoti, waumini wawili walijeruhiwa vibaya wakati wa kisa hicho cha kutamausha. News24 inaripoti kuwa kisa hicho kilitokea muda mfupi kabla ya saa usiku.

Ripoti zinaonyesha kuwa Wakristu 50 walikuwa wamekusanyika katika kanisa lao kwa ajili ya maombi na kukesha wakati majambazi hao wenye silaha walipowashambulia.

Inasemekana kuwa majangili hao walitoroka na mali zao za thamani kama vile simu na pesa taslimu.

Watu watatu akiwemo pasta walipigwa risasi wakati wa shambulio hilo na kukimbizwa kwenye kituo cha afya cha karibu, lakini pasta alifariki dunia alipofika hospitalini. Waathiriwa wengine wawili wanasemekana kuwa katika hali sawa.

Msemaji wa polisi wa Diepsloot, Luteni Kanali Mavela Masondo alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa msako wa kuwasaka wahalifu hao umeanzishwa. Vile vile aliongeza kuwa kesi za mauaji na jaribio la kuua zimefunguliwa.

"Watu watatu waliopigwa risasi, akiwemo mchungaji, walipelekwa katika kituo cha matibabu cha eneo hilo ambapo pasta alifariki alipofika. Wengine wawili wako katika hali mbaya lakini inaendelea vizuri."

Nyandarua

Katika kisa sawia na hicho, wezi walivamia Kanisa Katoliki katika kaunti ndogo ya Ol-Joro Orok, Nyandarua, na kutorosha vifaa vya thamani ya zaidi ya KSh 170,000.

Majambazi hao walivamia kanisa hilo usiku wa Jumamosi, Julai 16, na kuiba kinanda, meza na vitu vingine vya thamani.

Kulingana na mmoja wa wasimamizi wa kanisa hilo Gerald Gituta, majambazi hao waliingia katika jengo la kanisa hilo wakitumia silaha hatari.

Vijana hao walikuwa wamefika katika eneo la kanisa kujiandaa kwa ibada ya Jumapili, Julai 17, na kupata vyombo hivyo havipo.

Uchunguzi wa polisi umebaini kuwa huenda majambazi hao walitumia funguo feki kuingia kanisani ambako vifaa hivyo vilihifadhiwa kwa kawaida.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live