Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji aliyesema sio dhambi kuwa na 'mchepuko' kama Daudi kwenye Bibilia

5fdab78affacb786 Mchungaji aliyesema sio dhambi kuwa na 'mchepuko' kama Daudi kwenye Bibilia

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Mhubiri ambaye ni raia wa Ghana, Osofo Acheampong, ametoa kauli nzito kwa kusema kwamba sio vibaya kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando hata ingawa ni mume wa mtu.

Pasta Osofo Acheampong wa kuoka Ghana, alitangaza kwamba ni vizuri kwa mwanamume kuwa na mpango wa kando. Mhubiri huyo anayedaiwa kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa mfano wa Abrahamu na Daudi waliokuwa watumishi wa Mungu ilhali walikuwa kwenye mahusiano na wanawake wengi.

Video hiyo aliyosambaza mhubiri huyo iliibua msisimko kwenye mitandao ya kijamii.

Pasta Acheampong, anayesemekana kuwa kiongozi wa Kanisa la Kipentekosti la Sabato, alitoa maoni hayo kwenye mahojiano ya hivi punde huku akitoa mafungu ya Bibilia kuipa uzito kauli yake.

''Ni vizuri kuwa na mpango wa kando. Iwapo nitaipa alama, ni asilimia 100,'' pasta huyo alisema.

Pasta huyo alitoa mfano wa Abrahamu na Daudi ambao walimtumikia Mungu licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake nje ya ndoa. Alisema, hao walikuwa ni makuhani waliokuwa na mipango ya kando ilhali walikuwa ni watumishi wa Mungu.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke