Sakata la mchungaji mmoja nchini Uganda (jina limehifadhiwa) aliyefunga kanisa baada ya kushinda Sh100 milioni kwenye mchezo wa bahati nasibu, limewaibua viongozi wa kiroho huku kila mmoja akija na mtazamo wa tofauti.
Machi 16, mwaka huu mtandao mmoja Uganda ulichapisha taarifa za mchungaji huyo akieleza kuwa ameamua kufunga kanisa lake ili afanye shughuli nyingine kwa kuwa amepata fedha nyingi.
Mtandao huo ulimnukuu mchungaji akieleza namna alivyocheza bahati nasibu ya Sh1 milioni lakini akashinda Sh100 milioni ambazo hakutarajia kama angepata.
“I must admit that I opened this church due to greed but not anointing (lazima nikiri nilifungua kanisa hili kwa sababu ya ‘uchoyo’ lakini sio upako) inasema sehemu ya habari hiyo ikimnukuu mchungaji huyo.