Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Mackenzie na wenzake kuendelea kushikiliwa kwa mwezi 1 zaidi

Mchungaji Mackenzie Na Wenzake Kuendelea Kushikiliwa Kwa Mwezi 1 Zaidi Mchungaji Mackenzie na wenzake kuendelea kushikiliwa kwa mwezi 1 zaidi

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mchungaji mwenye utata ambaye pia ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya Shakahola Paul Mackenzie ataendelea kushikiliwa hadi Disemba 22 mahakama itakapotoa uamuzi kuhusu ombi lililowasilishwa na upande wa mashtaka kutaka kumweka kizuizini yeye na mwenzake kwa miezi 6 zaidi.

Akifikishwa mahakamani, Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka ya Umma Jami Yamina alielezea hofu kwamba washtakiwa wanaweza kujiua ikiwa wataachiliwa.

Muda wa nyongeza, alisema utaruhusu polisi kukamilisha uchunguzi kuhusu suala hilo.

Wakati ukitoa kesi yake, upande wa mashtaka ulidai kuwa Katiba inaruhusu kuzuiliwa kwa washukiwa wa ugaidi kwa hadi siku 360.

Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka ya Umma alisema kuwa Bunge pia limeidhinisha uamuzi wa kuongeza muda wa kuwekwa kizuizini kutoka siku 90 hadi siku 360 katika kesi tata.

Yamina katika hoja yake pia alipinga uamuzi wa mahakama wa kuwaachilia washukiwa 6 kati ya 29 kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na Idara ya Huduma za Baadaye.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka ya Umma, washukiwa hao watahitaji kufanyiwa mpango wa kuondokana na msimamo mkali, ikimaanisha kuwa watahitaji kufundishwa jinsi ya kuyakabili maisha kwa njia tofauti.

Kulingana na Yamina mpango huo utawasaidia kabla ya kuunganishwa tena katika jamii.

Paul Mackenzie anakabiliwa na mashtaka ya ugaidi kutokana na mauaji ya zaidi ya watu 300 kupitia dhehebualiloongoza kwa mahubiri ya upotoshaji.

Mchungaji huyo mara kadhaa amenyimwa dhamana na anaendelea kuzuiliwa na mamlaka.

Chanzo: Bbc