Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Mackenzie anakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo mauaji

Mchungaji Mackenzie Na Wenzake Kuendelea Kushikiliwa Kwa Mwezi 1 Zaidi Mchungaji Mackenzie anakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo mauaji

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya, Renson Ingonga ameidhinisha mashtaka 10 dhidi ya mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie , wa kanisa la Good news Internatioanal,anayetuhumiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 430 eneo la Shakahola ,pwani ya nchi hiyo.

Kiongozi wa mashtaka amesema baada ya kutathmini faili ya uchunguzi kutoka idara ya upelelezi ,kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki mchungaji Mackenzie na washirika wake 95 wanaohusishwa na vifo vya washirika wa kanisa hilo la kufunga hadi kufa.

Baadhi ya mashtaka dhidi ya Mackenzie ni mauaji na ugaidi mashtaka mengine yakiwa ni kuua bila kusudia na kusababisha majeraha ya mwili.

Kwa mujibu wa sheria ya Kenya ya kuzuia ugaidi na uhalifu wa kupangwa,watuhumiwa hao watashtakiwa kwa kuhusika kwenye uhalifu wa kupangwa na mafunzo yenye itikadi kali.

Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya AP Aidha chini ya sheria ya kuwalinda watoto ,Mackenzie na washirika wake watakabiliwa na kosa la ukatili dhidi ya watoto na ukiukaji wa haki ya kupata elimu.

Mackenzie na watuhumiwa wenzake wamekuwa korokoroni tangu mwezi mei mwaka uliopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live