Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchungaji Amlaumu Rais Kenyatta kwa Kusambaa kwa Corona

Mhubiri.png?fit=750%2C470&ssl=1 Mchungaji Amlaumu Rais Kenyatta kwa Kusambaa kwa Corona

Tue, 30 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mchungaji Amlaumu Rais Kenyatta kwa Kusambaa kwa Corona March 30, 2021 by Global Publishers



Siku kadhaa baada ya serikali ya Kenya kuweka vikwazo vikali dhidi ya biashara na usafiri katika majimbo matano ili kuzua kuenea kwa virusi vya corona, mhubiri mmoja jijini Nairobi, amemlaumu Rais Kenyatta kwa kuchukua hatua hiyo.

“Wewe [Rais Kenyatta], na wanasiasa wenzako mnafaa kulaumiwa kwa kueneza wimbi la tatu la corona,” alisema Askofu Peter Ambuka kutoka kanisa la Pefa katika eneo la Kahawa West viungani mwa jiji la Nairobi. Aliongeza kuwa Wakenya wengi sasa wanateseka kutokana na vikwazo hivyo kutokana na “hatua hiyo ya kutojali”.

“Nyinyi mnaendela kuishi kwa starehe kwa kutumia kodi yetu wakati tunapoteza chanzo cha mapato yetu ,” Askofu Ambuka alisema.

Alisema kuwa wakati viwango vya maambukizo vilipungua mwishoni mwa mwaka jana, Rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walianzisha tena kampeni yao ya kubadilisha katiba, ambayo ilivutia umati mkubwa.

Naibu Rais William Ruto, anayepinga mabadiliko hayo, pia alifanya mikutano mikubwa. Mikutano hiyo ilichangia pakubwa ”kueza virusi,” Askofu alisema.

Askofu huyo pia alisema kwamba hatua za hivi punde zilizochukuliwa na rais hazitoshi na huenda zikawaweka Wakenya katika mzunguko wa kufungiwa na amri za kutotoka nje.

Chanzo: globalpublishers.co.tz