Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchina aua kisa usaliti, ahukumiwa kifo

Geng Quandong And Girlfriend Used Ton Illustrate The Story Mchina aua kisa usaliti, ahukumiwa kifo

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Nigeria, imemuhukumu Mfanyabiashara wa China Frank Geng Quarong (49) adhabu ya kifo baada ya kumkuta na hatia ya kumuua mpenzi wake.

Mnamo mwaka 2022, Marehemu Ummu Kulthumu Sani aliyekuwa na umri wa miaka 22 alikutwa chumbani kwake akiwa amechomwa mara kadhaa na kitu chenye ncha kali huku mpenzi wake akiwepo.

Mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu alikuwa kwenye mahusiano na Mfanyabiashara huyo kwa takribani miaka miwili.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa familia, wawili hao walikuwa na ugomvi na binti huyo hakutaka kuendelea na mahusiano hayo.

Kesi hiyo ya mauaji iliishtua Nigeria na imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu sana.

Ni nadra sana kwa adhabu ya kifo kutolewa nchini Nigeria. Bw. Quarong amepewa siku 90 kukata rufaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live