Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji mwingine afuata nyayo za Mesut Ozil kutetea Waislamu China

89689 Ozil+pic Mchezaji mwingine afuata nyayo za Mesut Ozil kutetea Waislamu China

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Wellington, New Zealand. Nyota wa mchezo wa rugby wa New Zealand, Sonny Bill Williams amefuata nyayo za kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil kuikosoa China kuwa inainyanyasa jamii ndogo ya Uighur, huku akilaumu kuwa kuna baadhi ya watu wameweka fedha mbele kuliko "utu". Wakati lawama kwa Ozil kutokana na kitendo cha kuilamu China kuwa inanyanyasa Waislamu zikiendelea, Williams -- ambaye ametwaa Kombe la Dunia mara mbili akiwa na New Zealand na ambaye amebadili dini na kuwa Muislamu -- amelipa uzito zuala hilo. "Ni muda mbaya wakati tunapoweka mbele faida za kiuchumi dhidi ya ubinadamu," ameandika nyota huyo katika akaunti yake ya Twitter, kukiwa na mchoro unaoonyesha mkono uliona bendera ya China ukiubana mwingine wenye bendera ya "East Turkestan" --dhana inayotumiwa na wanaharakati wa Uighur kumaanisha jimbo la Xinjiang ambalo jamii hiyo inaishi -- huku kukiwa na damu. China ilijibu kwa hasira mashambulizi ya Ozil dhidi ya sera za taifa hilo ambazo zimefanya lilaumiwa na makundi mengi ya kupigania haki za binadamu na wataalamu wanasema wameona ukiukwaji wa haki za binadamu ukienea na watun wanaokadioriwa kufikia milioni moja wa jamii ya Uighurs na wengine, hasa Waislamu, wakifungwa. Ozil aliondolewa katika mchezo maarufu wa kompyuta wa soka wa Pro Evolution wa toleo la Kichina na televisheni ya serikali ya China iliondoa matangazo ya moja kwa moja ya mechi baina ya Arsenal na Manchester City. Katioka tukio kama hilo, mwezi Oktoba China iliiadhibu klabu ya Houston Rockets inayoshiriki Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA) baada ya meneja wake, Daryl Morey kuandika katika akaunti yake ya Twitter akiunga mkono waandamanaji wanaodai demokrasia wa Hong Kong.

Chanzo: mwananchi.co.tz