Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji aliyefia uwanjani azua kizaazaa Nigeria

98644 Pic+mchezaji Mchezaji aliyefia uwanjani azua kizaazaa Nigeria

Wed, 11 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kifo cha beki wa klabu ya Nsarawa United inayoshiriki  Ligi Kuu nchini Nigeria, Chineme Martins akiwa uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Katsina United kimezua kizaa zaa kikubwa nchini humo.

Mchezaji huyo alipatwa na mauti baada ya kugongana na mchezaji wa timu pinzani wakati wa kugombania mpira wa kona mwishoni mwa kipindi cha pili cha mchezo huo ambao timu yake ilishinda 3-0.

Taarifa zinasema Chineme alifariki dunia baada ya kufikishwa Hospitali aliyopelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu jiji la Lafia nchini humo.

Wakati tukio hilo linatokea kulikuwa na tatizo la kutokuwepo kwa gari la wagonjwa katika uwanja huo, hivyo utaratibu wa kumtoa uwanjani hapo kumpeleka hospitalini ulichelewa.

Siku moja baada ya taarifa hizo za kifo cha mchezaji huyo kutoka, Shirikisho la soka nchini humo (NFF), limeanzisha uchunguzi wa kuangalia hali ya vifaa vya matibabu katika viwanja vyote vya Ligi Kuu.

Kampuni ya Ligi imesimamisha Ligi hiyo na kueleza kuwa iwapo kuna viwanja vitabainika kuwa havijakidhi viwango, havitaruhusiwa kuandaa mechi za Ligi Kuu zilizobakia.

Pia Soma

Advertisement
Pia wamewataka makamishna watakaopangwa katika mechi husika kuhakikisha wanasimamia hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz