Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchezaji Yanga asajiliwa Rwanda

050b8d21722d3805dc404fbff8c2ba36 Mchezaji Yanga asajiliwa Rwanda

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

ERIC Rutanga, msimu ujao ataichezea timu ya Polisi inayoshiriki Ligi Kuu ya Rwanda, baada ya mpango wake wa kusajiliwa na Yanga kugonga mwamba.

Kwa miezi kadhaa kumekuwa na hali tofauti kwa beki huyo ambaye aliondoka Rayon Sports Mei na kutua timu ya Polisi na mwezi mmoja baadae alitangaza kutakiwa na Yanga.

Iliripotiwa mchezaji huyo alikubaliana na timu hiyo ya Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili, ukiachilia kando baadhi ya taratibu ambazo zilikuwa zikiendelea kukamilishwa ili aichezee klabu hiyo.

Taarifa za sasa zinasema mpango huo sasa umekufa na mchezaji huyo ameamua kurudi katika timu ya Polisi. Kwa mujibu wa CIP Maurice Karangwa, Katibu Mkuu wa Polisi, uhamisho wa Rutanga umekwama baada ya kutokea mabadiliko katika klabu ya Yanga, ikiwemo kumtupia virago aliyekuwa kocha wao Mbelgiji, Luc Eymael.

“Yanga walikuwa na matumaini mchezaji huyo angeichezea na pande hizo mbili tayari zilishafikia makubaliano ya awali, lakini mabadiliko ya hivi karibuni katika klabu (Yanga) yamefanya mpango huo kutokamilika,” alisema Karangwa na kuongeza:

“Sasa atachezea kwetu (kama tulivyokubaliana awali) kwa miaka miwili ijayo.” Rutanga anajiunga na Polisi baada ya kuitumikia Rayon kwa miaka miwili, ambako alishinda mara mbili taji la Ligi Kuu ya Rwanda na kufikia robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2018 akiwa the Blues.

Chanzo: habarileo.co.tz