Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchana watu ni wengi" Rais Uhuru atoa sababu za kuzindua hospitali siku

1432de046cfb2b19 Mchana watu ni wengi" Rais Uhuru atoa sababu za kuzindua hospitali siku

Wed, 7 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Rais Uhuru Kenyatta alisema ingelikuwa vigumu kwake kuzindua miradi mchana kwa sababu ya kanuni za COVID-19 Uhuru pia alisema kuwa alifungua hospitali hizo usiku ili ziweze kuhudumu kwa saa 24Wakati huo huo alizielekeza hospitali za umma jijini Nairobi kutoa huduma saa 24 ili kuhakikisha wakazi wanahudmia wakati wowote

Rais Uhuru Kenyatta ameelezea sababu za kuamua kuzindua miradi ya maendeleo usiku badala ya mchana kama ilivyokuwa desturi.

Akiwahutubia wanahabari jijini Nairobi, Jumanne, Julai 6, Kenyatta alisema ingelikuwa vigumu kwake kuzindua miradi mchana kwa sababu ya kanuni za COVID-19.

“Tulienda usiku kwa sababu tulitaka kuhakikisha kuwa tunafuata kanuni za COVID-19. Lakini kama muonavyo, ingelikuwa vigumu kuenda kufanya kile tumefanya leo wakati wa mchana kwa sababu ya umati wa watu," Uhuru alisema.

Uhuru pia alisema kuwa alifungua hospitali hizo usiku ili ziweze kuhudumu kwa saa 24.

“Zahanati hizo na hospitali zitatoa huduma saa 24 ili kupunguza msongamano katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta na Mama Lucy. Badala ya mtu kutumia nauli kuenda kutafuta matibabu katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, wanatakiwa kutafuta huduma katika vituo hivyo karibu nao,” Uhuru alisema.

Hospitali ambazo zilifunguliwa usiku na rais ni Hospitali ya Gichagi-Kangemi, Zahanati ya Gatina na hospitali zingine katika mitaa ya Mukuru Kwa Rueben, Tassia Kwa Ndege and Our Lady of Nazareth in Mukuru Kwa Njenga.

Rais ambaye alikuwa ameandamana na Mkurugenzi Mkuu wa NMS, Mohammed Badi na viongozi wengine pia alizielekeza hospitali za umma jijini Nairobi kutoa huduma saa 24 ili kuhakikisha wakazi wanahudmia wakati wowote.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke