Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato uanzishwaji kituo cha jeshi la Russia nchini Sudan wakamilika

Jeshi Maji Majia Mchakato uanzishwaji kituo cha jeshi la Russia nchini Sudan wakamilika

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Sudan imekamilisha marekebisho ya makubaliano yanayohusiana na kuanzishwa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini humo na kubainisha kuwa upande wa Russia umetimiza masharti yote muhimu ya kukamilishwa makubaliano hayo.

Shirika la Habari la Kimataifa la Tasnim, limenukuu taarifa hiyo ikisema jana Jumapili, kwamba viongozi wa Sudan wamekamilisha marekebisho ya makubaliano ya kuanzishwa wa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini humo wakisema kuwa, serikali ya Russia imetatua wasiwasi waliokuwa nao viongozi wa Sudan katika upande wa kijeshi, hivyo makubaliano hayao yameidhinishwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergei Lavrov alitembelea Sudan wiki iliyopita kwa safari ya kikazi. Siku ya Jumatano, shirika la habari la Bloomberg liliripoti kuwa ziara ya Lavrov nchini Sudan, iliyoambatana na ziara ya wawakilishi wa Umoja wa Ulaya na Marekani, ilikuwa ya kushitukiza kwa nchi za Magharibi.

Shirika hilo lilibainisha kuwa, kuwepo kwa wakati mwafaka mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Russia huko Sudan kulionyesha kuongezeka ushindani kati ya Kremlin na washindani wake barani Afrika.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na waziri mwenzake wa Sudan, Ali al Sadiq Ali, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Lavrov alikosoa vikali namna nchi za Magharibi zinavyozinyonya na kuzidhulumu nchi zinazoendelea na kuziwekea mashinikizo hata katika maamuzi yao juu ya nani wa kushirikiana naye na nani wa kutoshirikiana naye.

Ikumbukwe kwamba makubaliano ya kuanzishwa wa kituo cha jeshi la wanamaji la Russia nchini Sudan yalitiwa saini mwezi Desemba 2020. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Russia itaweza kupeleka zaidi ya wanajeshi 300 na meli zaidi ya nne kwenye kituo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live