Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mchakato kutumia sarafu moja EAC wafikia patamu

A5f177dccb8855a852546c71e32096be.jpeg Mchakato kutumia sarafu moja EAC wafikia patamu

Tue, 2 Mar 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MCHAKATO kuanzishwa sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unazidi kusonga mbele baada ya kuamuliwa kuundwa kwa Taasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki ifikapo Julai Mosi mwaka huu.

Uamuzi huo umefanywa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kikao chake kilichokaa wiki iliyopita, ikiwa ni mwanzo wa kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa makubaliano, EAC imeazimia kufikia matumizi ya sarafu moja ifikapo mwaka 2024 kama Itifaki ya Umoja wa Fedha (Sarafu) Afrika Mashariki inavyosema.

Baraza la Mawaziri katika mkutano wake wa 40 liliielekeza Sekretarieti ya EAC kuitisha Mkutano wa Baraza la Kisekta la Fedha na Uchumi Afrika Mashariki ili kuunda muundo wa taasisi ya pamoja ya fedha (EAMI) ifikapo Septemba 30, mwaka huu.

EAMI ni utaratibu wa mpito kwa Benki Kuu ya Afrika Mashariki ambao utatoa sarafu moja.

Baraza hilo pia liliagiza Sekretarieti kuanzisha mchakato wa kutambua washirika wa taasisi hiyo kulingana na taratibu za EAC.

Mkutano wa 19 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Kampala, Uganda Februari 23, 2018 ulilielekeza Baraza la Mawaziri EAC kuharakisha kuanzishwa kwa taasisi ya pamoja ya fedha ndani ya jumuiya.

Katika mkutano wao wa kawaida wa 20 ambao ulifanyika Arusha Februari Mosi, 2019, wakuu wa nchi za EAC waliridhia muswada wa uanzishwaji wa taasisi hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz